Google PlusRSS FeedEmail

PRO -24 DJS WAMLETA DNA




PRO -24 Dj’s wameanda tamasha linaloitwa ‘East Afrika pamoja concert’ litakalofanyika tarehe 30 mwezi huu , katika viwanja vya Dar Live tamasha hilo litapambwa na msanii kutoka nchini Kenya 'DNA' anayetamba na kibao kinachojulikana Banjuka na ‘Unamaswali  kwani wewe ni Polisi’

Katika tamasha hilo wasanii wa hapa nchini watapata fursa ya kufanya shoo ya pamoja na msanii huyo ili kuongeza radha tofauti ya muziki wa Afrika Mashariki

Pro-24 Djs wanaamini kuwa wanakazi kubwa ya kukuza taswira ya muziki wa Tanzania kwani kazi yao ni kutambulisha nyimbo pamoja na kumtambulisha msanii, hivyo hiyo ni njia moja wapo ya kuukuza muziki wetu Kwa njia hiyo ya kuwaleta wasanii tofauti wa nje wanaamini wanakuza muziki kwani msanii huyo anakuja na changamoto ambazo wasanii wa bongo wanajifunza mambo mengi ya muziki

PRO- 24 Dj’s ndio kundi la Kwanza la madj nchini Tanzania walioacha kutumia CD katika shughuri zao za muzki na kuendeleza kupiga muziki kwa kutumia vifaa vya kisasa vya Technic Turntable System na Serato vinavyounganishwa na kompyuta

Kundi hili la Madj ambawo wanapiga muziki wa aina mbalimbali katika kumbi tofauti tofauti za starehe pamoja na kuandaa matamasha huku wakiwaleta wasanii wa nje ya nchi kuja kufanya shoo katika ardhi ya Tanzani

Pamoja na hayo kinachowatofautisha Pro-24 Djs na Madj wengine ni kile kitendo cha wao kufanya shoo zao kwa kutumia zaidi mfumo wa kisasa pamoja na kupiga shoo livehuku kukiwa na full shangwe za mashabiki wao kuonyesha kukubali kile kinachofanywa na madj hao

Mbali na hayo katika harakati za kukuza muziki wa nchi yetu Pro -24 Djs wanawaleta wasanii wanaofanya vizuri wa Afrika Mashariki, wakiamini kuwa wanaleta changamoto katika tasnia hiyo ya muziki

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging