JACQUE PENTZEL AJICHIMBIA ZANZIBAR KUIPIKA FILAMU YAKE MPYA
Msanii mwenye mvuto wa aina yake katika tasnia ya filamu nchini Jacque Pentzel yuko kwenye maficho kwa mda mrefu sasa akiwa anaipika muvi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘HoneyMoon’
Msanii huyo ambaye ameamua kujichimbia kisiwani Zanzibar katika hoteli moja ya kitalii inayojulikana kwa jina la Shabar
Jacque alipata bahati ya kuzungumza na Maisha alieleza kuwa ameamua kujichimbia kwenye kisiwa hicho akiamini kuwa ndio sehemu rasi inayoendana na maudhui ya movi yake
Alisema kuwa yote hayo ni kwa ajili ya kutafuta utofauti wa filamu yake na nyingine ambazo zimezoeleka kuchezwa katika maeneo yale yale ya siku zote
“Mtu anaangalia movi lakini anakuwa anajua kabisa eneo hili ni wapi na wakitoka kuonyesha sehemu hii wataonyesha sehemu nyingine kwa hiyo mtazamaji anakuwa anajua maeneo ya hoteli , hii ni kwa sababu hatutaki kubuni mazingira mazuri kwa ajili ya kuboresha movi zetu” alisema
Aliongezea kuwa movi hiyo kunatofauti kubwa sana lakini ya kwanza ni mazingira yaliyofanyiwa kazi hiyo ambayo ni mazingira harisi