Google PlusRSS FeedEmail

TSHALA MWANA PROFILE


 Leo tunatua nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasiya ya Kongo DRC ambapo tunakutana na mwanamama Elisabeth Tshala Miana ,mwanamama huyo ni miongoni mwa wanamuziki wa kike barani Afrika wenye historia ndefu katika tasinia ya muziki wa kiafrika

Kwa mujibu wa historia yake Muimbaji huyo raia wa DRC zamani Zaire alizaliwa mjini Lubumbashi mnamo mwaka 1957,Tshala alianza kazi yake ya muziki mnamo mwaka 1976 mjini Kinshasa akiwa mnenguaji wa bendi mpya kwa kipindi hiko ya M’pongo Love ambapo baada ya miaka miwili akiitumia bendi hiyo aliamua kujiunga ya Minzoto Wella ambapo nako alikaa miezi michache akiwa mmoja wa wanafunzi wa Abeti Maskini

Akiendelea na kibarua chake cha kuimba hakuachana nacho hadi alipoondoka Congo Kinshasa ambayo na kwenda kutafuta maisha Ivory Coast. Mwaka 1981 akiwa mjini Abidjan mwanamama huyo alianza kuimba akiwa na bendi moja iliyokuwa ikiongozwa na raia wanchi hiyo

Hata hivyo kama ilivyoada kwa wasanii wengi husani wanamuziki umaarufu wa mwanadada huyo ulipatikana pale alipotua mjini Paris akiwa na mwanamuziki Hyacinthe, wakiwa na nyimbo zao kama ‘Amina’ wimbo ambao ulikuwa na miondoko ya Pop na ambao uliimbwa kwa lugha ya kifaraza ukisaidiwa na mwingine wa ‘Tshebele’ ambao ulikuwa kwenye maadhi ya mutuashi ambalo asili yake ni kabila La Baluba waishio kusini mwa DRC ndizo zilizompaisha mwanamuziki huyo

Inaelezwa kuwa albamu na matamasha mbalimbali ambayo bendi hiyo iliyafanya ndani na nje ya Ivory Coast ndiyo yalimfanya yazidi kumpaisha katika tasinia hiyo , mwaka 1984 Tshala alihamia mjini Paris ambako teyari eneo hilo lilishakuwa kituo cha kutayarisha nyimbo kwa wanamuziki wa kizaire

Akiwa mjini Paris alifanikiwa kurekodi albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la ‘Kami’ akiwa na raia wa Cameroon Aladji Toure na Kisha baadaye akarekodi albamu nyingine mbili Mbanda Matiere (Tatizo la wapinzani) na nyingine aliyoipa jila la M’Pokolo kwa lugha ya kifaransa, Le petiti Ruisseau likiwa ni maana kwa lugha ya Kiswahili mkondo mdogo

Albamu hiyo ya M’Pokolo iliandaliwa na mwanamuziki Toure wakimshirikisha mpiga gitaa mashuhuri raia wa Kongo DRC ,Rigo Star,hata hivyo mara nyingini Tshala alikuwa akijiiandikia kazi yake tofauti na ilivyo kwa wanamuziki wa kizaire kupendelea kuimba kwa lugha ya kilingala na kucheza mtindo wake wa rumba na ule wa Soukous , Tshala aliibuka na mtindo wake wa mutuashi ambapo kwa mara ya kwanza aliimba kwa kutumia lugha ya Tshiluba

Akiwa ameshajijenga jina ndani ya Abidjan na Paris, mwaka 1986 Tshala alirejea mjini Kinshasa na kujiandalia matamasha yake binafsi , hata hivyo licha ya kupata mapokesi makubwa baada ya kuwasili nchini humo tatizo la uchumi kuwa mgumu lilimfanya ashindwe kuendelea na kibarua chake nchini humo na hivyo kumlazimu Tshala kubaki makao yake makuu yakiwa mjini Paris ambapo walau kila mwaka aekuwa akifyatua albamu moja huku akifanya ziara Ulaya na Afrika



Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging