Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WAANZA UJENZI WA AWAMU YA PILI


 Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), umesema pamoja ya kusuasua kwa michango ya wanachama wake kuchangia ujenzi wa makazi yao katika kijiji cha Mwanzega wilayani hapa, awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba kumi umeanza.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza na wanachama katika kijiji cha Mwanzega waliokwenda kutembelea ujenzi huo, alisema ujenzi wa awamu ya pili umeanza kwa nyumba za gharama ndogo zaidi wa sh. milioni 3.8 ambao kutakuwa na baraza, chumba cha kulala, choo na jiko kwa ajili ya wanachama ambao uwezo wao ni mdogo.

Alisema ujenzi huo umeanzishwa baada ya wanachama kushindwa kuchangia ujenzi wa nyumba za sh. mil. 6.4, ambapo nyumba tano zilijengwa kati ya hizo, mbili zilinunuliwa na wanachama wawili kwa njia ya ofa.

Mwanachama Josephina Joseph akizungumza nyumbani kwake Mwanzega, Mkuranga baada ya kukabidhiwa nyumba yake alisema SHIWATA imempatia nyumba ambayo hakutegemea kupata zawadi hiyo na kushauri wanachama wengine waamini kuwa michango yao ndiyo itawapatia nyumba za kuishi.

"Nawashauri wanachama wenzangu wa SHIWATA, kuchangamkia ujenzi wa nyumba kwa sababu manufaa yake yanaoneakana wazi mfano ni wangu," alisema Josephina.

Katika uzinduzi wa awamu ya pili wa nyumba hizo wanachama zaidi ya 100 waliohudhuria uzinduzi huo, wamemsifu mwanachama mwenzao Manase Kikapu kwa kuanzisha kilimo cha mbogamboga katika kijiji hicho.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging