Kitendo kilichofanywa na wasanii wawili wanaotamba katika soko la filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kupanda jukwaani huku wakionesha sehemu kubwa ya maungo yao ya mwili vimeonekana kuwakera wadau mbalimbali wa tasnia ya sanaa nchini
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mwenyekiti wa Chama cha Watunzi wa Miswaada ya Filamu Tanzania (TASA) Abdul Lihinda alisema kitendo hiko kinadharilisha soko la filamu Tanzania na tasnia nzima ya filamu
Alisema kama msanii ni kioo cha jamii na wanajamii wanategemea mambo mengi mazuri kutoka kwako hivyo kinachofanyika ni kudharirisha tasnia hiyo
Aliongezea kuwa kitendo hiko kimewakasilisha pia hata Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) na teyari hatu za awali zimeshachukuliwa kwa kuwaandikia barua wasanii hao wawili ambayo barua nyingine imepelekwa wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na hatua nyingine zinaendelea kufuatwa ili kukomesha uchafu huo