Shirika la kimataifa linalo husiana mambo ya afya(PSI) ikishirikiana na Shirikisho la Filamu(TAFF) pamoja na Chama cha waandishi na watunzi wa miswada ya filamu Tanzania(TASA) kwa pamoja wameandaa shindano la kutafuta miswada bora ya filamu kwa mwaka 2012.
Hayo yalizungumzwa jana Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama cha waigizaji Tanzania Bw.Abdul Maisal ambapo alisema kuwa kuanzishwa kwa shindano hilo kuna sababu nyingi zikiwemo kutoa elimu kwa jamii juu ya vvu,kuimarisha umoja wa wasanii hapa nchini kupitia shindano na nyinginezo.
Aidha alisema kuwa shindano hilo lilianza rasmi jana kwa kuongea na waandishi kisha kwanzia septemba 24 mwaka huu utakuwa ni muda wawashiriki kuchukua fomu za maombi ya ushiriki ambapo washiriki wote watatakiwa kurudisha fomu pamoja miswada Octoba 30 mwaka ctoba 30 mwaka huu.
Bw.Maisal alisema kuwa kutakuwa na kamati ya kufanya uchambuzi wa miswada iliyokidhi viwango vya kwenda katika ushindani na uchambuzi huo utafanyika octoba 31 wakati Novemba 10 itakuwa ni siku ya fainali ya shindano hilo.
Pia alisema kuwa miswada yote itakayo ingizwa katika shindano hilo itafanyiwa ukaguzi kutokana na mujibu wa sheria ya filamu na michezo Tanzania kifungu namba 4 ya mwaka 1976 inayosimamiwa na bodi ya filamu Tanzania.
Alimalizia kwa kutaja mahali fomu hizo zitakapo patikana kuwa ni katika ofisi za shirika la filamu Tanzania zilizopo magomeni moroco zilizopo jirani na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya kinondoni.