WIZ KHALIFA :ANATAMANI KUITWA BABA
Rapa wa Marekani Wiz Khalifa amesema atafurahia kama siku moja atazaa na mpenzi wake mwanamitindo Amber Rose
Kauli hiyo imechukuliwa kama kuunga mkono kauli ya Amber ambaye alidaiwa anataka kumzalia mtoto wake wa kwanza rapa huyo
Wiz na Amber kwa nyakati tofauti kila mmoja ameshazungumzia hali hiyo jambo linaloleta maneno ya chini chini kuwa mrembo huyo tayari anaujauzito
Lakini wawili hao kila mmoja hakuna aliyeweza kuthibitisha juu ya jambo hilo kwa kuwa hawataki kulizungumzia kiundani hata wakiulizwa
Wiz alisema "Nataka siku moja kuitwa baba, naamini Amber ipo siku atatimiza hilo na tutakuwa na familia yetu yenye amani na furaha kama ilivyo sasa"