BIEBER AKATISHA SHOO JUKWAANI BAADA YA KUUGUA GHAFLA
Msanii chipukizi wa miondoko ya Pop kutoka nchini Marekani Justine Bieber ameugua ghafla na kukatisha shoo aliyokuwa akifanya
Tukio hilo lilitokea wakati msanii huyo alipokuwa akiimba moja ya nyimbo zake wakati yupo katikati ya kushusha mistari aliugua ghafla na kulazimika kukatiza shoo hiyo
Bieber alikuwa akiimba kwenye tamasha lililofanyika katika mji wa Glendale, Arizona ambalo lilikuwa kati ya tamasha kubwa lililowahi kutokea nchini Marekani
Kwa mujibu wa msimamizi wa tamasha hilo alisema kuwa msanii huyo aliondoka jukwaani baada ya tukio hilo, lakini alirejea baada ya muda mfupi wa mapumziko
Baada ya kupanda tena jukwaani Bieber aliwauliza mashabiki wake "Je mtanipenda japokuwa nitakuwa nipo katika hali iliyonitokea hivi karibuni juu ya jukwaa?"
Baadae msanii huyo aliandika katika ukurasa wake wa kijamii Twitter kuwa "Maziwa yalikuwa siyo chaguo lake sahihi lo!"