Akihojiwa na shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC akiwa Afrika ya Kusini alisema kuwa wasanii waliokwisha toka wanamsaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kwa urahisi kazi zake za sanaa
Alisema kuwa alishirikiana na wasanii mbalimbali wa kimataifa akiwamo Juliana Kanyomozi wa Uganda pamoja walitoa baadhi ya nyimbo zilizopendwa
Msanii huyo ambaye aliwahi kufanya kazi za sanaa nchini Uganda kwa miezi miwili alisema kuwa ameamua kuweka maskani yake Afrika ya Kusini kwa kuwa nchi hiyo ipo juu katika tasnia ya muziki