RUSHWA YA NGONO YATAWALA TASNIA YA FILAMU
Rushwa ya ngono yatawala tasnia ya filamu nchini ambapo imeelezwa kuwa baadhi ya wasichana hutoa rushwa ya ngono ili wapate nafasi ya kuingia katika tasnia hiyo
Hayo yalibainishwa na muigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu nchini Yvonne Sherry 'Monalisa' alisema kuwa rushwa imetawala katika tasni hiyo kwa baadhi ya wasichana kuamini kuwa hawawezi kutoka katika tasnia hiyo bila ya kutoa rushwa ya ngono
Monalisa amewasikitia baadhi ya wasichana kwa kutumia vibaya miili yao ili waweze kuingia katika tasnia hiyo badala ya kutumia kigezo cha vipaji vyao
"Mwanzoni nilikuwa siamini kama kulikuwa na vitendo kama hivyo vya rushwa ila baada ya kuchunguza nikagundua kama rushwa imejaa sana katika tasnia nzima" alisema
Aliongezea kuwa baadhi ya watu waliamini kuwa watayarishaji wa filamu ndio wanaowashawishi wasichana kutoa rushwa ya ngono ila si kweli kwani wasichana hao ndio wa kwanza kujipeleka wakiamini kuwa watapata nafasi
Monalisa alisema kuwa hata kama ukijipeleka kingono bado kipaji ndicho kitakufanya uendelee kuwepo katika tasnia hiyo na si kitu tofauti na hicho
Alitoa mwito kwa baadhi ya wasichana ambao wanania ya kuingia katika tasnia hiyo ya filamu wanatakiwa kuamini kipaji chao na kuwa wavumilivu huku wakijichua katika mazoezi ndio njia ya wao kujiibua kisanii na si kutafuta njia ya rushwa kwani mwisho wao watachezewa
Aliongezea kuwa tasnia ya filamu ni ndogo hivyo waandaji wa filamu pia ni wachache kwa hiyo wasichana wasipokuwa makini watachezewa na kushindwa kupata kile wanachokihitaji