Mwanamuziki wa siku nyingi wa muziki wa kizazi kipya nchini Anselm Tryphone maarufu kama Soggy Doggy amesema kuwa anajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa mwanzilishi wa Bongofleva hapa Nchini
Soggy ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Uhuru Fleva cha Uhuru Fm alisema kuwa waanzilishi wengi bado wanafanya vizuri na bado wanaheshimiwa kutokana na kazi zao zenye uhakika, tofauti na wengine wanaoingia na kutoa nyimbo moja inatamba kisha heshima yake inashuka baada ya muda mfupi"Najivunia kuwa mmoja wa waanzilishi wa huu muziki na bado nawaona wasanii wengi wapya hawana jipya hasa wanaoimba Hip pop maana hata nisipotoa nyimbo mpya bado heshima yangu mtaani iko juu sana "