Google PlusRSS FeedEmail

DULLY KUPAGAWISHA BILICANS JUMAPILI



Msanii maarufu wa bongo fleva nchini Tanzania, Dully Sykes anayetamba na vibao vingi ikiwemo Shikide, na sasa anatamba na 'mtoto wa kaliakoo'anatarajia kufanya shoo ya 'kufa mtu' ndani ya Club Bilicans jumapili ya tarehe 7 mwaka huu

Msanii huyo ambaye amejipanga kutoa burudani ya aina yake ndani ya ukumbi huo huku akiwa anajinadi kwa kuwaambia mashabiki wake wawe teyari kupokea vitu tofauti usiku huo, huku akisisitiza kuwa amejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wake

Alisema kuwa hajawahi kuwaangusha mashabiki wake hivyo amejipanga kwa ajili ya kufanya makamuzi ya nguvu na kusisitiza kuwa mashabiki wahudhurie ili kupata radha tofauti

Shoo hiyo ambayo imepewa jina la 'Usiku wa Club'itakayokuwa ikifanyika kila siku ya jumapili, kutakuwa na wasanii tofauti tofauti watakao kuwa wanafanya shoo ya kufanya mtu ndani ya club bilicans kwa kiingilio cha elfu 600

Shoo hiyo ambayo pia itarushwa live na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC 1) huku ikiwa imeandaliwa na Pro 24 Dj's

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging