ISHA MASHAUZI ATAWALA JUKWAA MASAA MAWILI DARA LIVE
Msanii wa taarabu ambaye anajiamini na haishiwi na vionjo kila kukicha Isha Mashauzi alionekana kuwapa burudani vilivyo mashabiki wake kwa kutumia muda usiopungua masaa mawili katika tamasha la 'East Africa Pamoja Concert' iliyoandaliwa na Pro 24 Dj's
Msanii huyo ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic alionekana kupania kufanya kweli baada ya kumiliki stage kwa muda usiopungua masaa mawili huku mashabiki kuonekana bado wanamuitaji jukwaani
Isha ambaye siku zote hujipanga kufanya shoo ya nguvu kwa kupanda na wacheza shoo wake huku wakionekana wako mahiri
Akizungumzia tamasha hilo Isha alisema kuwa hujipanga kwa ajili ya kufanya maangamizi ili mashabiki wake wapate kile kinachostahili
Alisema kuwa anawajali mashabiki wake kwa kuwapa vionjo vipya kila siku kwani kazi yake ni kutoa burudani kwa mashabiki wake