Ukizungumzia muziki wa reggae nchini Tanzania bila shaka utamtaja Jhikoman ambaye alitoa singo yake ya kwanza mnamo mwaka 94 ' Don't Bleach' ndio jina la singo yake
Kazi yake kubwa ni kuipa taarifa jamii inayomzunguka kuhusu mstakabi wa maisa ya kila siku, kwai anachokiimba ni maisha ya kila siku yanayomtokea mwanadamu kwa namna moja au nyingine
Jhikoman aliyipata nafasi ya kupanda jukwaa moja na msanii kutoka nchini Kenya DNA kwenye tamasha la 'East Africa Pamoja Concent'lililoandaliwa na Pro 24 Djs
Alisema kuwa kwake ni faraja kubwa kupanda jukwaani maeneo ya Mbagara na kuona watu wameukubali muziki wake kitu ambacho kinampa changamoto kubwa
Alisema kwamba alikuwa anasubili nafasi kama hiyo ya kufanya shoo mahali hapo ili watu wote waweze kufikiwa na ujumbe unaopatikana kwenye muziki wake
Akizungumzia sababu iliyomsukuma kuimba muziki wa reggae, anasema falsafa iliyomo ndani ya muziki huo ndio kikubwa kilichomsukuma yeye kuimba reggae
Anasema kuwa haigi kazi ya mtu yeye anaimba kile kinachohusu jamii hivyo anaigusa jamii ya Tanzania katika nyimbo zake
Pamoja na hayo alipongeza Pro 24 Dj kwa kile walichokiandaa kwani lengo ni kukuza muziki wa Tanzania pamoja na burudani kiujumla