Hii imemtokea Neyo mwaka 2008 kwani alipokea simu na kusikia upande wa pili ukijitambulisha kuwa alikuwa ni Michael Jackson, alikata simku hiyo na kuendelea kulala
Bahati nzuri mpigaji alipiga tena na aliposikia vizuri aligundua kuwa ni Michael Jackson akizungumza, Neyo alisema siku hiyo hakulala kabisa kwa furaha alichofanya ni kuwapigia marafiki zake mmoja baada ya mwingine kuwapa taarifa
MJ alimpigia akitaka kufanya naye kazi na walikubaliana kukutana siku mbili baadaye hata hivyo walichozungumza hakikufanikiwa kwani mwaka mmoja baadaye alifariki dunia