LAMAR AZINDUA ALBAMU YAKE YA KWANZA
Mwanamuziki Kendrick Lamar amezindua nyimbo zilizopo kwenye albamu yake ya kwanza inayoitwa Good Kid, m.A.A.d City, ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Octoba 22 mwaka huu. Albamu hiyo imerekodiwa na kampuni ya Top Dawg Entertainment na Aftermath/Interscope Records.
Katika albamu hiyo yenye nyimbo 12, Lamar amewashirikisha baadhi ya wanamuziki wa lebo ya Top Dawg akiwemo Jay Rock, Drake pamoja na Dr. Dre.
Watengeneza muziki (producer) Scoop Devillee, T-Minus, Rune Rask, na Just Blaze ndio watengenezaji pekee ambao wametajwa kuhusika kuitengeneza albamu hiyo.