FAT JOE WAMALIZA BIFU NA 50 CENT
50 Cent na Fat Joe ambao wamekuwa katika bifu kubwa kwa muda mrefu wameamua kumaliza tofauti zao wakati walipotoa heshima kwa Chris Lighty katika tuzo za BET Hip-Hop 2012.
Akiongea na kituo cha redio cha Hot 107.9 kiongozi wa Terror Squad Q Deezy alisema kuwa Lighty alijaribu mara kadhaa kuwapatanisha wawili hao bila kufanikiwa, lakini sasa yeye amefanikiwa kuwapatanisha.
“Mtu aliyenigundua mimi ndiye huyohuyo aliyemgundua 50 Cent namuheshimu sana Chris Lighty kwa sababu nilikuwa nikipata tabu sana wakati nikiwa Bronx.
Kila mmoja hupata kama miaka 75 ya jela, Mungu amjalie kwa sababu Chris aliokoa maisha yangu Sikuwahi kuamini kama siku moja ntakuwa rapa ila yeye alinifundisha kurapu na alitaka sisi tumalize tofauti zetu lakini tulimpuzia "
Joey Crack alisema kuwa alijua 50 Cent angekuwepo pale na mara alipofika ukumbini, 50 Cent alimnong'oneza kitu masikio kisha wakashikana mikono na kumaliza bifu lao.
"Nilikuja katika tuzo nilijua kuwa 50 cent angekuwepo lakini nilikuja kwa sababu ya kumuenzi Chris Wakati tuko pale, 50 cent aliniambia kitu masikioni mwangu katika hali ya kiungwana Maneno aliyosema ni kama mimi ni muungwana.
Siwachukii watu Mimi ni baadhi ya watu wachache sana wa Hip-Hop wenye mapenzi baada ya 50 kusema hayo, tulishikana mikono na kuamua kumaliza bifu. Ilikuwa ni kama vile watu wawili ambao wamekuwa na kuamua kusema, hii ni kwa ajili ya Chris. tuendelee na maisha yetu