SAJUKI, WASTARA KUWASHUKURU WATANZANIA
Tamasha kubwa la aina yake litakalowashirikisha wanamuziki wasanii wa filamu na watangazaji linatarajia kufanyika mjini Iringa jumapili ya wiki hii, kwa mujibu wa mwandaaji wa tamasha hilo Wastara Juma alisema tamasha hilo ni kwa ajili ya kuwashukuru watanzania kwa sala na michango katika kurejesha afya ya msanii huyo wa filamu za bongo Sadick Juma Kilowoko maarufu kama 'Sajuki'
Wastara alisema kuwa katika tamasha hilo kundi la bongo movies litakuwepo kutoa sapoti kundi hilo litasakata ndinga na watangazaji wa Iringa kama sehemu ya tamasha








