SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA
Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini pia ni msanii wa sanaa ya vichekesho (comedy) Hussein Mkiety anayejulikana kwa jina la Sharo Milionea amefariki dunia kwa ajari ya gari iliyotokea mkoani Tanga muda wa saa mbili usiku
Akithibitisha ajari hiyo kamanda wa polisi wa kimkoa wa Tanga, Bw. Constatine Masawe alisema kuwa ajari hiyo ilitokea majira ya saa mbili usiku maeneo ya kijiji cha Lusanga Muheza ambapo pia ni nyumbani kwa marehemu akitokea Dar es Salaam akielekea Tanga
Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali teule ya Muheza mkoa wa Tanga, MUNGU AMLAZE MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA








