C9 "SIJAPATA WA KUZIBA PENGO LA SHARO MILIONEA'
PRODUCER anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya Charles Francis anajulikana kama C9 ambaye pia ndiye aliyemuibua marehemu Shalo Milionea amekiri kuwa yupo katika kipindi kigumu kwa kutafuta msanii ambaye atakayeweza kuziba pengo la marehemu Shalo milionea katika kazi ya muziki
Ugumu huo anaupata kwa sababu ya aina ya muziki huo na alitumia muda mrefu kumtengeneza Shalo mpaka kuweza kuimudu stair hiyo na kuweza kuitendea haki
Aliyasema hayo wakati akielezea jinsi gani baadhi ya wasanii wa hapa nyumbani wanavyofanya kazi kwa kuigana huku wakishindwa kuwa wabunifu na kupoteza ualisia wa kazi za sanaa
Alisema kuwa tatizo kubwa lipo kwa baadhi ya wasanii kwa kuwa na uwezo mdogo na kukosa ubunifu kwenye kazi zao kwa kushindwa kuwa na ubunifu wa hali ya juu ili waweze kuteka soko la muziki
"Msanii anakuja studio anakwambia anataka kurekodi nyimbo kama ya fulani kwa sababu alimsikia msanii mwenzie anaimba na anahisi na yeye akirekodi kama hivyo itafanya vizuri, kitendo hiko kinasabababisha msanii asahau nini maana ya sanaa kwamba ni ubunifu" alisema C9
Aliongezea kuwa tatizo ambalo maproducer wengi wanakosea ni kuchukua wazo la msanii la kuiga beat ya msanii mwenzie na kuifanyia kazi wakati kazi ya producer ni kumshauri msanii ili kuweza kuboresha muziki
C9 alisema tabia ya baadhi ya wasanii kuigana mawazo ya nyimbo linasababisha kudumaza muziki na siyo kukuza muziki katika soko la kimataifa








.jpg)