Google PlusRSS FeedEmail

KOSOVO : "WANAMUZIKI WA TANZANIA WATUMI KISWAHILI KUJITANGAZA"




Wanamuziki wa Tanzania wanabahati kwa kuwa kiswahili ni lugha ya taifa na sasa lugha hiyo inakuwa kwa kasi huku watu wa mataifa mbalimbali wanaonekana kuvutiwa na lugha hiyo lakini wanamuziki hawaitumi vizuri bahati walionayo kwa kuwa wabunifu katika kazi zao

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na mwanamuziki wa bendi Ndanda Kosovo, wakati akielezea hali ya muziki wa dansi nchini huku wasanii wakionekana kushindwa kutumia vizuri lugha ya kiswahili katika kujipandisha kimuziki

Alisema kuwa wasanii wanatakiwa watumie lugha ya  kiswahili katika kukuza na kuendeleza muziki wa tanzania pamoja na kutumia vyombo vya habari kama BBC Swahili kwa ajili ya kutangaza muziki wa tanzania inayoimbwa kwa lugha ya kiswahili ili waweze kuteka soko la muziki

Kosovo alielezea sababu zinazopelekea wanamuziki wa bendi wa nje kufanya vizuri kuliko wa nyumbani ni pamoja na kuwa na wakurugenzi ambao ni wanamuziki, hali hiyo ni tofauti na bendi za nyumbani ambapo wakurugenzi wanakuwa hawajui chochote kuhusu muziki ila yuko hapo kwa ajili ya maslahi yake binafsi na si kuendeleza muziki

"Mkurugenzi hajui chochote kuhusu muziki zaidi ya kuangalia anaingiza kiasi gani cha fedha na ndio maana baadhi ya wanamuziki wa bendi wanaishi kwa kuomba omba kwa kuwaimba wadau ili wapate pesa" alisema Kosovo

Alisema kuwa wanamuziki wa dansi wanatakiwa wawe wabunifu kwani tangu mwaka 1999 hakuna kilichobadilika kumbi na ratiba ni zile zile hakuna kitu kipya ambacho kinaleta mabadiliko katika muziki wa dansi

Pamoja na hayo Kosovo alisema kuwa ameshatoa albamu inayojulikana kwa jina la 'Focus' ambayo inafanya vizuri sana nchi kama Boswana, Zambia na kupata mialiko ya shoo kubwa tofauti na nchini

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging