JE NI KWELI SISTA P NI MJAMZITO ?
Hatimaye msanii machachari Sister P amepata ujauzito unaonekana kumsumbua kwa kipindi kifupi huku akishindwa kufanya kazi zake kama awali
Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa msanii huyo ujauzito wake ni mchanga lakini unaonekana kumsumbua sana 'kwa kutema tema mate ovyo', na kuchagua chakula, huku wakati mwingine kushindwa kufanya kazi zake kama awali
"Anadalili kabisa za mimba tena mimba changa kwa kusumbua, na yeye anasumbuka sana ila bora kaamua kubeba mimba maana ni muda mrefu na miaka inazidi kwenda hajapata mtoto" kilieleza chanzo hicho
Mwandishi wa habari hii alimtafuta Sister P ili aweze kudhibitisha ukweli wa habari hizo, yeye alisema kuwa ni kweli anaonekana kwa baadhi ya watu kama na dalili ya ujauzito kwa sababu ya kutema mate ovyo na muda mwingine kukaa karibu na chombo cha kutemea mate
Aliendelea kusema kuwa kuna wakati anachoka sana na anashindwa kula hivyo watu wake wa kalibu wanapomuona na hali kama hiyo hudhani huenda akawa na mimba changa
"Huwana nashindwa kula kabisa na nina tema sana mate kwa kipindi hiki, na hata ninapo toka kwenda katika mizunguko yangu huwa nina beba chombo cha kutema mate kwani nashindwa kujizuia" alisema Sista P
Alisema kuwa hizo ni dalili za ujauzito na ndio maana watu wake wa karibu hudhani kuwa yeye ni mjamzito,
Aliongezea kuwa kama akiwa na mimba haitojificha na kuna siku kila mtu ataiona hivyo kwa sasa amekataa kuliweka wazi swala hilo kama ni kweli anamimba au la







