MSETO EAST AFRICA KIMEONGOZA KWA KUNYAKUWA TUZO TATU
Uongozi wa kipindi cha Mseto East Africa kinachorushwa kila siku ya Jumatatu na Citizen television kimetoa shukurani zao za dhati kwa mashabiki wao kwa kuwasababishia kupata ushindi kwa kunyakuwa tuzo tatu za Coast Music Awards
Akizungumza kwa niaba ya uongozi huo katika kipindi hicho mtangazaji maarufu toka nchini Kenya Willy Tuva alisema kuwa wanatoa shukurani zao za dhati kwa mashabiki wao wote kwa kuwapigia kura kwa wingi na kusababisha ushindi wa tuzo hizo tatu kwa mwaka huu
Alisema kuwa wanafuraha kwa kuona kipindi chao kinachounganisha East Afrika kwa ujumla kuweza kunyakuwa ushindi na kuonekana ni kipindi bora zaidi
Pamoja na hayo alitoa wito kwa wadau wa sekta ya muziki kushirikiana kwa pamoja ili kukuza muziki wa East Afrika uendelee kufanya vizuri ulimwenguni kote
Kipindi cha Mseto East Africa ni kipindi kinachorusha video mbalimbali za muziki za wasanii kutoka East Afika Kenya, Tanzania, Uganda








