Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ,Leo Ijumaa Dec 21 inatarajia kumsomea mwenendo wa kesi ya mauaji inayomkabili msanii maarufu wa filamu nchini Elizabeth Michael "Lulu"Msanii huyo anayedaiwa kumuua Steven Kanumba,Leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika mahakama hiyo ili kusikiliza mwenendo wa upelelezi wa kesi yake,chini ya hakimu Agustina Mmbando.Mshitakiwa huyo atasomewa mwenendo huo wa kesi tayari kwa kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam..Mapema wiki hii upade wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika ,kwa mujibu wa hati ya mashitaka ,Lulu anadaiwa April 7 mwaka huu,Eneo la sinza Vatican Dar es salaam,Mshitakiwa alimuua Kanumba,Kanumba alizikwa April 10 mwaka huu katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam mazishi yaliyohudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa wa selikali na vyma vya siasa..
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.