Google PlusRSS FeedEmail

BARNABA "SORRY NI KWA AJILI YA MASHABIKI WANGU"




Msanii mwenye mvuto wa kipekee anayetamba na ngoma kali za kimapenzi Barnaba Elias a.k.a baba Steven amefunguka na kuelezea maudhuhi yaliyobebwa kwenye nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Sorry' ambapo anatarajia kuzindua video ya nyimbo hiyo mwishoni mwa wiki

Akizungumza jijini Dar es Salaam Barnaba alisema kuwa nyimbo yake ya 'sorry' ni maalum kwa mashabiki wake wote kwani ni neno linalotumika kwa kila mtu hususani kwa kipindi hiki cha kufunga mwaka

Alisema kuwa sorry ni neno dogo lakini limebeba maana  kubwa kwa mtu anayejua maana tena linapunguza machungu na hata kurudisha upendo ambao ulikuwa kwenye hatari ya kutoweka kwa ajili ya makosa mbalimbali

Alisema kuwa neno hilo linatumika na watu wa lika tofauti tofauti hususani kwenye kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kila mtu anajaribu kumuomba mwenzie msamaha kwa kutumia neno hilo hivyo nyimbo yake inaishi na maisha halisi ya binadamu kila siku

"Kila mtu sasa anatamka sorry nyimbo yangu inatumika kuwafariji watu mbalimbali kwa kuamini neno sorry ndilo pekee lenye kuleta faraja katika maisha ya kila siku " alisema Barnaba

Aliongezea kuwa anatarajia kufanya uzinduzi hivi karibuni wa video yake huku akihakikisha kuwa enaendana sambamba na ujumbe uliobebwa kwenye nyimbo hiyo

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging