Google PlusRSS FeedEmail

KOFFI OLOMIDE AWATAKA WAIMBAJI WA BENDI WA HAPA NYUMBANI KUJIAMINI





MUIMBAJI nguli kiafrika wa muziki wa dansi kutoka nchini Kongo Charles Antoine Koffi Olomide amewapa mashabiki wake wa Tanzania nafasi katika moyo wake ikiwa ni moja ya njia ya kuwashukuru kwa upendo na ukarimu waliouonyesha kwake

Koffi Olomide ambaye alikuja nchini kwa ajili ya tamasha la Tusker Carnival alisema hayo wakati wa shoo yake iliyofanyika Leader Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Muimbaji huyo ambaye alionekana kutamani kuzungumza kiswahili ili aweze kuwasiliana na watanzania waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo,hata hivyo alitumia wasaa kuwatambulisha washiriki wa kumsaka mrembo anayegombania taji la Miss East Africa

Kofii amabaye alikuja na kundi zima la Quartier Latin alikonga nyoyo za mashabiki wengi waliohudhuria tamasha hilo kwa kuimba vibao mbalimbali vilivyomo katika albamu yake ya nyuma iitwayo Affaire D'Etat

Mbali na hayo Kofii alitoa wito kwa waimbaji wa muziki wa bendi nchini kujiamini na kuamini kile wanachokifanya ili waweze kufikisha muziki wa tanzania kuweza kujulikana duniani kote

Katika kunogesha tamasha hilo bendi kadhaa za nyumbani ikiwemo Mapacha watatu, Diamond Musica, Twanga Pepeta pamoja na Skylight Band zilialikwa kufanya makamuzi ya  nguvu huku bendi ya Diamond Musica kuonekana kuja kivingine wakiwa na nguvu mpya kwa kufanya kweli stagen huku wakiibua hisia tofauti kwa mashabiki wao









This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging