Google PlusRSS FeedEmail

C9 ATAMANI KUFANYA KAZI NA LADY JAY DEE



PRODUCER wa muziki wa kizazi kipya Charles Francis C9 ambaye pia ndiye aliyemuibua marehemu Shalo Milionea anatamani kufanya kazi na Lady Jay Dee kwa sababu ya uwezo aliyonao msanii huyo

Alisema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa anaelezea mikakati yake ya mwaka ujao jinsi ya kuboresha na kuendelea kuwa mbunifu katika kazi zake

Alisema kutokana na kipaji na uwezo aliyo nao msanii Jay dee anatamani siku moja afanye naye kazi na anaamini itakuwa ni kazi nzuri ambayo watanzania wataipokea na itafanya vizuri katika soko la muziki ndani na nje ya tanzania

Alisema kuwa si kila msanii mwenye jina au ambaye teyari ameshapata mafanikio anatamani kufanya naye kazi bali ni msanii pekee mwenye uwezo na nidhamu katika kazi ndiye anayempa kipaumbele kwanza

"Natamani sana kufanya kazi na Jay Dee kwa sababu ya kipaji chake ni kikubwa mbali na kipaji chake pia anaheshima katika kazi kitu ambacho kinanifanya niweze na nitamani kufanya naye kazi siku moja " alisema C9

Aliongezea kuwa wasanii ili wafike hatua ya maendeleo hususani wa muziki wanatakiwa wawe na heshima ya muda na kazi kwani kwa kutofanya hivyo wtakuwa wanajirudisha nyuma kimaendeleo wenyewe

Pamoja na hayo alielezea kuwa yupo mbioni kuendeleza mipango yao ya kazi ambayo walikuwa nayo kabla marehemu Shalo Milionea kufariki ikiwemo ya kusaka watu wenye uwezo wa kuimba stairy ailiyokuwa anafanya marehemu






This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging