Google PlusRSS FeedEmail

MAJUTO AFUNGUKA TANGAZO LA AIRTEL




KUTOKANA na malalamiko ya  baadhi ya mashabiki na hali ya kutofahamu juu ya sababu inayosababisha kuendelea kuonyeshwa kwa tangazo la kampuni ya simu ya mkononi Airtel lilikouwa limerekodiwa na marehemu Sharomilionea, King Majuto afafanua sababu zinazosababisha  tangazo hilo kuendelea kuwa hewani kwa kipindi hiki

Akizungumza kwa njia ya simu Amri Athumani a.k.a King Majuto alisema kuwa mkataba bado unaendelea kuwepo na ndio maana bado tangazo hilo linaendelea kuchezwa katika vyombo vya habari

Alisema kuwa mbali na mkataba huo pia mama yake mzazi na marehemu Sharomilionea ameomba tangazo hilo liendelee kupigwa ili kwa kipindi cha mwezi mmoja ili aweze kupata fedha za kujikimu kimaisha kwa kipindi hiki ambacho mwanaye ndiye alikuwa msaada mkubwa kwake

"Tangazo hilo linapigwa kwa makubaliano ya mama yake mzazi ili aweze kupata fedha za kujikwimu , na ameruhusu lipigwe kwa kipindi cha mwezi mmoja na ndio maana unaona linachezwa hilo tangazo katika vyombo vya habari" alisema King Majuto

Mbali na hayo alipouulizwa mwanasheria wa kujitegemea Mwemezi Makumba  juu ya uhalali wa kuendelea kulicheza tangazo hilo yeye alieleza kuwa,kama taratibu zote zilifuatwa na kukamilika katika mkataba huo ni halali kuendelea kucheza tangazo hilo huku mafao pamoja na stahiki zote za marehemu zikilipwa kwa mrithi wake

Alisema kuwa kulingana na taratibu za mkataba kukamilika mtu anapokufa na mkataba haufi, bali unaendelea kwa kushirikisha warithi wa marehemu

Aliongezea kuwa mkataba unaweza kufa kama taratibu za mkataba huyo haujakamilika kisheria

This entry was posted in

3 Responses so far.

  1. Unknown says:

    nyie mnao hoji ni kinanani na mnataka nini toka kwa tangazo ilo la sharo , kama mnanjaa pelekeni gerezan na si kwa familia ya sharo ,ndugu tu wamekubali tangazo liendelee nyie vip tena ,hizo njaa kafieni mbelee mbwa nyie!!

  2. WABONGO Bwana, sasa walizani ngugu hawaoni au???? harafu pia kuna kalenda zinatoka zina picha za marehem, sasa nalo hili familia imeruhusu hili kufanyikaa?????

  3. Anonymous says:

    Jaman mbona mastaa wetu wa bongo wakifa wengi huacha habari mbaaaya na tukiwaona barabarani wanaonekana maisha yao na familia zao saaaafiii!!!!???@@**

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging