MUSTAPHA ATAMANI KUONGEZA TATOO KATIKA MWILI WAKE
Msanii anayetamba kwa kasi katika anga za muziki nchini Kenya Colonel Mustapha amefunguka juu ya michoro ya tatoo katika mwili wake inampa utata kwa baadhi ya mashabiki wake
Akizungumzia hilo jijini Nairobi Mustapha alisema michoro hiyo inamaana kubwa sana katika mwili wake na bado ataendelea kuongeza michoro mingine, kwani anapenda kuwa na michoro tofauti tofauti katika mwili wake
Alisema kuwa hawezi kuweka michoro katika mwili wake usio na maana hivyo michoro yote inamaana kubwa katika maisha yake kiujumla
Alisema kuwa kuna mchoro kama Jahazi ukiwa unamaanisha kuwa maisha yake mungu ndiye anayeyapeleka na mchoro mwingine ni namba 8 ambayo pia ina maana kubwa katika maisha yake
Akizungumzia mchoro ambao umempa wakati mgumu ni mchoro wa 'demu analia' huku baadhi ya mashabiki wakidhani kuwa ndio tabia yake ya kuliza wasichana wengi
"Mchoro huu msichana analia umenipa wakati mgumu sana kwani baadhi ya watu wanadhani ni tabia yangu ya kuliza wasichana jambo ambalo si la kweli kwani nina upendo kwa watu wote" alisema Mustapha