MWANAMUZIKI RIVER AFARIKI DUNIA
Muimbaji mahiri kutoka nchini Mexico Jenni Rivera amefariki dunia kutokana na ajali mbaya ya ndege iliyotokea nchini humo mapema wiki hii
Rivera ambaye alikuwa maarufu zaidi nchini Marekani alikuwa na miaka 43 wakati alipokutwa na umauti huo
Baba wa Rivera na kaka yake ndio waliothibitisha kifo cha msanii huyo kilichotokea katikati ya mji wa Telemundo, katika ajali hiyo hakuna abiria hata mmoja aliyebahatika kupona
Rivera alikuwa akielekea katika mji wa Monterrey ambapo alikuwa na kazi ya kufanya tamasha usiku wa Jumamosi








.jpg)