Google PlusRSS FeedEmail

KUNDI LA 'NO NAME' WAMEACHIA 'HANDS UP




KUNDI la muziki linaloitwa 'No name' linaloundwa na producer wa bongo Records Paul Matthysse a.k.a P Funk Majani pamoja na maproducer wenzie John Mahundi, Dunga, Lamar na Karabani wameachia single ya kwanza inayojulikana 'Hands Up' ikiwa ni moja ya mpango wa malengo yao ya kutangaza muziki kimataifa

Kundi hilo lililoundwa miaka 18 iliyopita na P Funk pamoja na Karabani mwaka huu wameamua kulifufua na kuongeza nguvu kwa kuwaongeza maproducer wengine watatu ili kuufikisha muziki wa kitanzania katika mataifa mbalimbali

Akizungumza jijini Dar es Salaam P Funk alisema kuwa kundi hilo lina lengo moja la kukuza muziki na kufanya muziki ujulikanane kote ulimwenguni

Alisema kuwa wanafanya muziki wa kila aina ambayo itawekwa kwenye santuri moja na kuuzwa kote nchini,  ikiwa na maana mgeni anapofika na kutaka kupata radha ya muziki wa tanzania atakuwa na kila sababu ya kununua santuri hiyo itakayobeba muziki tofauti tofauti

"Ukinunua Santuri yetu utapata muziki wa kila aina Afro Pop, Ragga, Bongo Fleva, Tradition kila aina ya muziki utapata ndani ya Cd moja ambapo tunataka kutanga muziki Afrika na nje ya Afrika" alisema P Funk

Akizungumzia hali ya muziki unavyokwenda kwa kipindi hiki alisema kuwa anashangaza na maproducer ambao hawajui kutafuta soko la muziki

Alisema kuwa yeye ni mtafutaji na anauchungu na muziki wa bongo felva kwani ameutoa mbali muziki huo na anatamani siku moja ufike kwenye ngazi ya kimataifa

Alisema kuwa siku hizi hakuna msanii anayeweza kuzindua albamu na kujaza watu kama kipindi cha nyuma, na kutolea mfano wa Juma Nature ambaye alizindua albamu ya Ugali aliyofanya Diamond jubly na kuweza kuja mashabiki wengi ambapo mpaka sasa hakuna msanii aliyeweza kuvunja rekodi yake

"Msanii akitoa single moja anazindua club huko nako hapati hata watu, tofauti na wakati ule nimeweza kuupigania muziki kwa kiwango kikubwa lakini maproducer wengi wa sasa hawajui wajibu wao kwenye tasnia hii ya muziki" alisema P Funk

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging