RIHANNA ASAIDIA HOSPITALI BIL. 2.7/-
Rihanna atoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya zaidi ya dola milioni 1.75 (sh.bilioni 2.7) kwenye hispital ya nyumbani kwao Barbados
Ametoa mchango huo kupitia mfuko wa hisani wa Clara Lionel Foundation ambao umepewa jina la bibi na babu yake, Clara na Lionel Brathwaite
Rihanna alikuwa na urafiki wa karibu sana na bibi yake ambaye alikuwa akimwita Gran Dolly. baada ya bibi huyo kufariki katikati ya mwaka huu, alimkumbuka kwa kuchora tatoo ya malaika wa Kimisri aitwaye Isis katikati ya kifua chake