TWANGA PEPETA KUFUNGA MWAKA KIVINGINE
Bendi ya African Star 'Twanga pepeta'inatarajia kufanya bonanza la kuaga mwaka 2012 litakaloshirikisha bendi ya Msondo Ngoma pamoja na vikundi vya burudani likiwemo kundi la muziki wa taarab la Mashauzi Classic
Hayo yalisemwa na meneja wa ASET Hassan Rehani na kufafanua kuwa bonanza hilo litafanyika jumapili ambapo pia bendi hiyo itatambulisha nyimbo tatu mpya za 'Nyumbani ni Nyumbani', Ngumu kumeza, na kila nifanyalo
Meneja huyo alivitaja vikundi vingine vilivyoalikwa kwenye bonanza hilo kuwa ni Hisia Cultural Group, Wakali sisi, Twanga Academy pamoja na msanii wa filamu Dokii
Aliongezea kuwa mwaka ujao watauanza kwa wimbo mmoja utakaounganishwa na zile zilizokamilika kwa ajili ya albamu ya 12 ambayo awali ilipangwa kuzinduliwa mwaka huu
Alisema kuwa wanajiandaa kuongeza wimbo mmoja kwenye albamu hiyo kufuatia muimbaji wao wa zamani Mwinjuma Muumin kuhama na wimbo wake wa 'Mapambano kipato'