SAJUKI HOI ALAZWA ICU
Afya ya msanii wa filamu nchini Juma Kilowoko 'Sajuki' inazidi kuwa mbaya ambapo inadaiwa amewekewa mashine ya gesi kwa ajili ya kumsaidia kupumua katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU Muhimbili
Habari hizo zimesibitishwa na katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Wilson Makubi kwa kusema kwamba bado afya yake si nzuri
Makubi alisema kuwa leo TAFF itakwnda Ikulu kufwatilia safari ya msanii huyo ili aweze kupelekwa India kwa matibabu
Alisema serikali imechukua jukumu la kumhudumia msanii huyo ambaye anatarajia kuondoka nchini mara baada ya taaratibu za safari kukamilika
Sajuki ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Mumimbili amegundulika kuwa anatatizo la figo na kwamba yupo chini ya uangalizi na uchunguzi zaidi
Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu ambapo mwaka jana aligundulika kuwa na uvimbe ulioanzia mikononi na baadaye ndani ya mwili, kwenye ini na sehemu tofauti za tumbo