Google PlusRSS FeedEmail

VITUKO VYA WASANII WA BONGO MWAKA 2012



 WAKATI zikiwa zimebaki siku chache tufunge mwaka 2012 na kuukalibisha mwaka 2013 baadhi ya matukio ya wasanii wenye majina yaliyojili na kushika kasi katika vyombo mbalimbali vya habari

Wasanii  maarufuku katika tasnia ya filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel ambao ni kioo cha jamii walishangaza jamii pale walipofanya kituko kikali cha mwaka kwa kucheza huku baadhi ya maungo yao nusu utupu juu ya jukwa katika Serengeti Fiestel

Baada ya tukio hilo wasanii hao walipoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari walikili kufanya hivyo na kukomaa kuwa hawatoacha kuvaa nguo fupi,lakini siku chache baadaye baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutoa maneno makali juu ya udharilishaji wa  tasnia hiyo walijikuta wakiwaangukia mashabiki wao kwa kuisogelea habari maelezo na kuomba radhi mashabiki wao kwa kupitia vyombo vya habari

Akinukuliwa wakati akiomba radhi Aunt Ezekiel alisema "Ni kweli nilikuwa ninacheza jukwaani lakini nilikuwa nimekunywa pombe sikuwa nimedhamilia kukaa uchu bali ni mbinu za wapiga picha ambao waliamua kutudharilisha na kupiga picha wakiwa chini ya jukwaa".

Mbali na vituko hivyo pia msanii Wema Sepetu atakumbukwa kwa tukio la aina yake ya kujalibu kufwata nyayo za marehemu Steven Kanumba kuzidi kuitangaza sanaa ya Tanzania nje ya nchi kwa kumleta msanii mwenye jina kubwa nchini Nigeria Omotola, huku akiwa na ndoto ya kutengeneza naye movi itakayomjengea jina zaidi na kuzidi kuitangaza tasnia hiyo.

Wakati huo huo msanii anayeendelea kuwika na kufanya vizuri katika anga za muziki wa kizazi kipya nchini Diamond  Plantumz alifanya kituko cha mwaka baada ya kutaka kuonyesha wadau usafi wake kwa kuvua nguo na kubaki na nguo ya ndani (boksa) nyeupe jukwaani huku akiwa ameambatana nawacheza shoo wake ambao wote walionyesha usafi wao kwa kuvua kama yeye.








Pia msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya pamoja na tasnia ya filamu nchini Baby Madaha naye kwenye fiesta mwaka huu alijikuta akipanda  stejini kwa mbwembwe na kujikuta akimwaga radhi kwa kuonesha matiti hadharani na kusababisha umati uliokuwa umefurika uwanjani hapo kulipuka kwa shangwe huku msanii huyo akiendeleza kufanya shoo kali bila ya kujali ile sehemu ya wazi aliyoiacha.

Tukio hilo la aibu isiyo na kipimo lilishuhudiwa na baadhi ya wadau na wanahabari usiku wa kuamkia Septemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako kulikuwa na tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2012.

Msanii huyo alijikuta akifanya kioja hicho  baada ya kutakiwa kupanda jukwaani kuimba na Juma Kassim ‘Nature’ ambaye wameshirikiana katika moja ya nyimbo zake.


Vile vile msanii anayechipukia katika tasnia ya kuigiza Isabela a.k.a "vai wa ukweli" alijikuta akilipotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuuza utu wake kwa kubaki utupu baada ya kufakamia pombe za bure toka kwa maswaiba wake wa karibu jijini Dares Salaam.

Muigizaji huyo aliandikwa baadhi ya vyombo vya habari kwa kujikuta katika tukio hilo akisaula nguo na kubaki mtupu kutokana na kuzidiwa kwa ulevi ambapo alikunywa zaidi ya uwezo wa kichwa chake

Isabela ambaye ameigiza filamu na mastaa kibao ambapo kati ya movie saba ambazo amewahi kucheza ni kama vile  Good fellow,2 eyes,Black Wear,Doa la maisha ,na Men day out

Kwa kuendeleza vituko na vioja baadhi ya wasanii walishindwa kuvumia na kuendeleza vituko vyao hadi katika msiba wa marehemu Steven Kanumba kwa baadhi ya wasanii wa kike kuonekana kushindwa kulia kwa sababu ya kuwa na kope za bandi

Wasanii ambao wanapenda kuwa na urembo wa kope za bandia kope hizo ziliwasababisha kushindwa kulia kwa kuhofia kope zao kutoka

Huku baadhi ya wasanii kuonekana kuzimia na simu zao za aina ya Blacbell kung'angania mikononi mwao, msanii Wema Sepetu alilipotiwa kuwa amezimia huku akiwa ajaiachia simu yake hiyo

Mbali na vitu hivyo baadhi ya wasanii wameendelea kuwa na vituko kwa kujihusisha kwenye mahusiano na vijana wadogo ambao wamewapa majina ya 'vijibwa'

Baadhi ya wasanii wameripotiwa kujihusisha na wavula wadogo kwenye mahusiano yao huku wakiwaita majina ya ajabu ajabu ili kuficha kwa baadhi ya watu katika jamii

Msanii analiyejipatiwa umaalufu kwa kupitia muziki wa kizazi kipya Shilole amelipotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa mwaka huu kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzie Barnaba huku akiwa anasikika akimwita kwa jina la 'kijibwa' kwa kuwa anamuudumia vitu vingi ili kudumisha mapenzi yao

Mbali na hayo baadhi ya wasanii wa kike pia wamekuwa na vituko kila kukicha kwa kujalibu kujibadilisha rangi 'kujichubua' ili waonekane tofauti na kuongeza urembo wao

wasanii ambao wamezidi kuonekana weupe tofauti na mwanzo ni msanii Wema Sepetu amabye ukimwangaali kwa macho ya kawaida utagundua tofauti kubwa ya rangi yake ingawa mwenyewe hajataka kuweka wazi zaidi kama anajichubua

Akinukuliwa wakati anazungumza na chombo kimoja cha habari jijini Dar es Salaam alipoulizwa kuhusu muonekano wake na kama anajichubua msanii huyo alikana kutumia mkologo na kuzidi kujiaminisha kuwa hatumii na hajawahi kufikiria kutumia kitu kama hiko

Shilole ambaye pia ni msanii anayekuja kasi zaidi anazidi kuonekana tofauti kwa kujitahidi kutumia mkorogo ingawa na yeye haishi na vituko kila awapo jukwaani kufanya shoo ambaye anaonekana akiwa anacheza kwa mitindo ya tofauti huku akiwa anaibuwa hisia tofauti za msahabiki wake





This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging