MRISHO 'PEKUPEKU' INANISAIDIA
MSANII wa miondoko ya kutohoa Mashairi Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la 'Mjomba' azidi kujipatia umaarufu kwa mashabiki wake kutokana na tabia yake ya kuimba jukwaani akiwa ajavaa viatu 'pekupeku'
Hali hiyo imeonyesha kuwashangaza mashabiki walio udhuria tamasha la Masupastaa wa filamu Tanzania lililofanyika mwishoni mwa wiki 'Dar Live' jijini Dar es Salaam
Akizungumza baada ya shoo hiyo juu ya kuto vaa viatu wakati akifanya shoo Mjomba alisema, amekuwa na mazoea ya kuto vaa viatu anapokuwa anafanya shoo ili kuwe na uhusiano baina ya nyayo zake na jukwaa
Alisema kuwa hapendi kufikiria ni kiatu gani avae kwani vimevaliwa vingi na bado hajaona thamani ya viatu hivyo, kwa hiyo ili kuepuka kufanya chagu la viatu vya kuvaa anapofanya shoo anaamua kupanda jukwaani akiwa hana viatu
"Naimba nikiwa sina viatu ili nipate hisia zaidi jukwaani, pamoja na hayo pia vimevaliwa viatu vingi sana ila sijaona kiatu cha tofauti hivyo basi kwangu viatu havina thamani sana niwapo jukwaani" alisema Mjomba
Mjomba alisema mbali na hiyo pia kuwa katika hali hiyo kwa upande wake ni utambulisho wake kwa mashabiki na wote wanaomfwatiria yeye
"Lazima mtu uwe na kitu kinachokutambulisha kama msanii mimi kupanda jukwaani nikiwa pekupeku ni moja ya utambulisho wa Mjomba " alisema Mjomba