MTINDO WA 'KIDUKU' UMEPOTEZWA NA 'KIBEGA'
UCHEZAJI wa aina ya 'kibega' ndio mtindo unaonekana kushika kasi huku ukitawala uchezaji wa watu wengi hali hiyo imesababisha kuupoteza mtindo wa 'Kiduku' ambao ulionekana kupendwa pia na watu wengi
Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini hivi karibuni alionekana kujimwaya mwaya miondoko ya 'kibega' na kundi la Makomando kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) hali hiyo inaonyesha staili hiyo kukubalika zaidi kwani mbunge huyo ni mmoja wa wabunge vijana ambao wanaunga mkono muziki wa bongofleva
Licha ya kuonekana akijimwayamwaya mbunge huyo anaonyesha jitihada za kuendeleza muziki wa kizazi kipya kwani yeye ndiye chanzo cha kuanzisha kundi la Kigomo all Star'ambalo linanyota wengi wanaofanya vizuri kwenye muziki huo
Staili hiyo ya kibega imeonekana ikipendwa na watu wengi hadi watoto huku ikisababisha kupotea kwa mtindo wa kiduku
Akizungumzia muziki huo mmoja wa kundi hilo lenye maskani yake Dar es Salaam Fred Felix a.k.a Fred Wayne alisema wanajivunia kuanzisha staili hiyo mpya huku ikiwa imeteka mashabiki wengi ndani na nje ya nchi
Alisema chanzo cha kutafuta staili hiyo ni kuwa tofauti na wasanii wengine hali ambayo iliwachukua muda na kushilikisha baadhi ya wasanii wengine ili kuboresha mtindo huo
"Mwenzangu ndiye aliyekuja na wazo hilo hivyo tulilifanyia kazi, pia tulimshilikisha msanii Joti ili kuboresha mtindo huo mpaka sasa staili hiyo inafanya vizuri" alisema Wayne
Kundi la Makomando, ndilo la kwanza kuanzisha miondoko ya kibega huku kundi hilo likiwa linaundwa na wasanii wawili Saidi Christopher 'Mucky' pamoja na Wayne








