DULLY AWATAKA WASANII WENZAKE KUIMBA 'LIVE'
WASANII wa Tanzania wanatakiwa kufanya shoo zao 'live' huku wakitumia vyombo na badala yake kuachana na kuimba kwa kutumia CD kwani inashusha uwezo wao wa kufanya shoo stage
Hayo yamezungumzwa na msanii wa bongo fleva anayefanya vizuri Afrika Mashariki Dully Sykes kwa kusema kuwa wasanii wa nyumbani wanapaswa kujiendeleza kwa kuanza kufanya shoo live
Dully ambaye alitamani wasanii wenzie kufanya kile anachokifikiria kwa maana ya kukuza na kujiendeleza kimuziki kwa kufanya shoo live huku wakitumia vyombo vya muziki kwa kufanya hivyo mashabiki watapata radha ya muziki wenye halisi na si kutumia CD ambapo inawapa ugumu mashabiki wao kila kukicha
Alisema ili tuendelee kimuziki lazima wasanii wakubali kubadilika, na kwa upande wa mapromota wanatakiwa kuandaa shoo live na kuwalipa wasanii wanaofanya live shoo na kuachana na mambo ya CD
"Kiukweli inabidi tubadilike kama tunahitaji kuendelea itapendeza sana kufanya shoo live na hapo ndipo uwezo wa msanii utakapoonekana kwani wengi wao kufanya live hawawezi " alisema Dully
Pamoja na hayo aliwataka wasanii kujifunza kupokea mabadiliko ya maendeleo ya muziki kwani wasanii wa nje wanafanya vizuri kulingana pia na shoo wanazozifanya wanaweza kufanya shoo live, kumiliki jukwaa na kuimba kwa umahili wa hali ya juu
" Wasanii wa nje wanauwezo wa kuimba kucheza kumiliki jukwaa bila ya tatizo lolote ila pia wamejifunza na wanapokea mabadiliko ya maendeleo mapema sana tofauti na wa hapa nyumbani hivyo tunahitaji kubadilika kila siku" alisema Dully
Nyota huyo alitoa wito kwa wasanii wenzie kwa yeyeto anayehitaji kujifunza vyombo ni ruhsa kwenda na kutumia vyombo vyake hii ni njia moja wapo na harakati za kukuza muziki wa kitanzania








