MWAKIFAMBA ASHANGAZWA NA BAADHI YA WASANII KUTOFIKA KATIKA TAMASHA
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF) Simon Mwakifamba ashangazwa na kitendo cha baadhi ya wasanii wa filamu kuchelewa na wengine kutofika kabisa katika tamasha la masupastaa wa filamu Tanzania
Mshangao huo uliibuka pale baadhi ya wasanii kuchelewa kufika katika tamasha hilo, na wengine kutofika kabisa akiwemo Ray pamoja na Wema Sepetu, hali hiyo imesababisha maswali mengi kwa mashabiki wake huku wengine wakioji ni sababu zipi zilizomfanya asitokee kwenye tamasha hilo
Akizungumza baada ya tamasha hilo Mwakifamba alisema hajapendezeshwa na kitendo cha wasanii kuchelewa kufika katika shughuri hiyo wakati ni ya kwao hivyo walipaswa kuwahi kufika
Alisema baadhi ya wasanii wanapenda kuchelewa kufika katika shughuri nyingi ili kuweka umakini kwa watu wanaowaangalia akiwa amefika mwisho, kitendo hiko wanakiona ni cha ufahari bila ya kujua wanaharibu soko
"Unajua wasanii bwana wanaona ufahari kuchelewa kwenye shughuri wanapenda wanapofika kila mtu wamuone kuwa amefika mapozi nini yaani bado hawako makini na muda kiasi ambacho maendeleo yanahitaji umakini na muda pia wao wala hawafahamu hilo na pia hawaonyeshi kujali" alisema Mwakifamba
Akizungumzia kama amepokea taarifa yoyote ya wasanii wasiofika kama Wema Sepetu na Ray ambao mashabiki walionekana kuwa na shauku ya kuwaona, Mwakifamba alisema hajapokea taarifa yoyote ili ya kutokufika kwao na ameshangazwa na kitendo hiko kwani wasanii wote waliofika wamelipwa
Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu wajitambue na baadhi yao kuacha utoto ili wafanye vitu vinavyoenda na wakati kwa manufaa ya filamu Tanzania
Tamasha hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki Dar Live jijini Dar es Salaam lilihudhuriwa na wasanii wa filamu pamoja na baadhi ya wasanii wa bongo fleva








