WASANII wa muziki wa bongo fleva wanaounda kundi la Makomando wanaotambulika kwa kuanzisha staili ya 'Kibega' Fred Felix 'Fred Wayne' pamoja na Saidi Christopher 'Mucky' washangazwa na wasanii wanaoamini kuwa na rasta 'dredi' ndio kukamilika kuwa msanii jambo ambalo wao wanaona si sahihi
Wanaamini kuwa ili ukamilike kuwa msanii lazima uwe na vitu tofauti tofauti ambavyo vitakavyo kutofautisha na wasanii wengine na kuonyesha upekee uliokuwa nao
Akizungumza kwa niaba ya mwenzake Fred Wayne alisema msanii anatakiwa kuwa mbunifu kwa kujitofautisha kwani wao kwa upande wao wanakuwa makini kwa kuongeza ubunifu kila wakati ili waonekane tofauti
Nyota huyo alieleza kuwa wao wanabadilisha mitindo ya nywele kila wakati huku wakiamini si lazima kuwa na staili ya dread kma wasanii wengine walivyozoea hivyo wao wameamua kuwa tofauti kwa kuwa na mitindo tofauti kila wakati
Alisema kuwa wao wameamua kuwa na staili ya tofauti kwa kusuka mitindo mbalimbali huku wakipaka rangi nywele zao ili kuongeza utofauti
"Wasanii wanaamini kuwa hauwezi kuwa msanii bila ya kufuga dread sasa sisi tunapenda kuonekana tofauti hivyo ndio maana tuna mitindo yetu amabayo ukituona kichwani hata kama tumekupa mgongo lazima utajua wale ni wa kina nani " alisema Wayne
Aliongezea kuwa kwa upande wake sasa ameamua kusuka na pembeni kunyoa kwa kuwa sasa anaimba tofauti na mara ya kwanza alivyokuwa 'dansa' aliamua kunyoa nywele zote na kuacha 'kiduku ' hali hiyo inamuonyesha utofauti wake wa mara ya kwanza na sasa
Kundi la Makomando linaundwa na wasanii hao wawili ambapo ni wasanii kutoka Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT) ambapo wapo hapo kwa ajili ya kujiendeleza kujifunza sanaa










