AMBER AJIACHIA NA WIZ
MWANAMITINDO mwenye makeke mengi Amber Rose ameonyesha mimba yake kubwa wakati wa utoaji wa tuzo za Grammy.
Amber aliweza kukatiza katika zulia jengundu 'Red Carpet' akiwa na mpenzi wake rapa Wiz Khalifa.
Amber, 29, alikuwa amevaa gauni jeusi ambalo linaonyesha kwa asilimia kubwa ukubwa wa tumbo lake.
Wawili hao walionekana kuwa ni watu wenye furaha na matarajio makubwa kutokana na jinsi wakati wote walivyoonyesha kuwa katika mapenzi mazito kama vile ndio wamekutana.








