Google PlusRSS FeedEmail

CHALZ BABA AGEUKIA MKWANJA




RAIS wa bendi ya Mashujaa 'wanakibega' Charles Gabriel 'Chalz Baba'  ameweka wazi msimamo wake wa kazi na kueleza kuwa yupo teyari kuhamia bendi yoyote ile yenye masirahi na dau kubwa la kifedha

Hayo yalielezwa na muimbaji huyo wa bendi ya Mashujaa  wakati akifafanua  uvumi ambao umeenea juu ya yeye kurudi tena katika bendi ya Twanga Pepeta yenye maskani yake jijini Dar es Salaam

Chalz Baba alieleza kuwa uvumi huo anausikia  kupitia kwa watu mbalimbali ingawa  bado hajakutana na viongozi wa bendi hiyo ya Twanga Pepeta na kuzungumza chochote kuhusu kurudi katika bendi hiyo

"Mimi nimesikia huo uvumi kuwa ninampango wa kurudi Twanga ila bado siajongea na uongozi rasmi, kwangu hakuna tataizo kama wana dau kubwa la kunilipa kuliko hapa nilipo narudi tu mimi ni kama kinyonga nabadilika kulingana na rangi" alisema Chalz Baba

Alisema yeye anatafuta pesa hivyo kama bendi hiyo imejipanga kumrudisha atarudi bila ya tatizo kwa dau kubwa kwani yupo kazini hivyo anaangalia maslahi

Aliongezea kuwa anafanya muziki kisasa hivyo anapopata mkataba mpya ukiwa na maslahi makubwa basi anauwezo wa kubadili mawazo

Chalz Baba alijifananisha kama mchezaji mpira anayebadilika kulingana na kiwango cha fedha anachopewa

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging