Kutokana na kitendo cha kupata ajali wakati akiwa njiani kuelekea studio mwanamuziki Chris Brown amtupia lawama paparazi aliyekuwa akimpiga picha mfululizo akidai kuwa kitendo hiko ndio chanzo cha ajali hiyo
Mwanamuziki huyo alisema kitendo cha kupigwa picha mfululizo wakati akiendesha gari kilimsababisha mawenge ambayo yalimfanya agonge ukuta
Katika ajali hiyo hakuna aliyeumia isipokuwa gari la mwanamuziki huyo aina ya Porsche liliharibika vibaya