MARIAH CAREY, NICK CANNON WAJIANDAA KUTAFUTA WATOTO
Wanamuziki Nick Cannon na Mariah Carey wamesema kuwa watautumia mwezi huu vizuri ili waweze kufikisha matarajio yao ya kupata watoto wengine waweze kuongeza familia licha ya Morrocan na Monroea ambao ni mapacha
Nick alisema makubaliano yao watahakikisha kuwa hadi mwezi huu unapomalizika watakuwa wameshapata matarajio ya kuongeza watoto kwenye familia hiyo
"Mwezi huu tumemuachia mlezi kazi ya kukaa na watoto sisi tunafanya jitihada za kuongeza familia " alisema Nick huku akicheka
Maria alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri kuwa mwezi huu ni wao akisema kuwa watoto watabaki nyumbani na dada wa kazi