Amini usiamini lakini ndicho kilichotokea. Muimbaji wa kike Rihanna juzi mchana alimsindikiza Chris Brown na mama yake Joyce Hawkins kwenda kusikiliza kesi ambayo inamkabili.
Chris Brown amefunguliwa mashitaka katika mahakama moja akituhumiwa kutomaliza adhabu ya kufanya kazi za kijamii aliyopewa kwa kosa la kumpiga Rihanna.
Mwendesha mashitaka wa Serikali anaitaka mahakama imuathibu Chris Brown kwa kosa hilo. Chris Brown anashutumiwa pia kwa kuwahonga polisi wa Virginia ili waseme kuwa mwanamuziki huyo alimaliza adhabu hiyo aliyopewa.
Vyanzo vya habari kutoka mahakamani vilipasha kuwa Rihanna alimrushia busu Chris Brown na kusema maneno mazuri ya kumuunga mkono.








