ROSE NDAUKA AFAFANUA UREMBO WAKE
Naye msanii wa filamu Rose Ndauka pia ameweka wazi kuwa kunywa maji kwa wingi pamoja na kupumzika ndiyo siri ya urembo wake
Alisema pia hata kufanya mapenzi anaratiba ili asiharibu mwili wake huo hivyo anazingatia sana hilo na ndio siri ya mafanikio yake
Msanii wa muziki wa bongo fleva Barnaba yeye alisema kinachomsababisha kuendelea kuonekana na afya njema na muonekano nadhifu ni kutotumia kilevi cha aina yoyote na kufanya juhudi katika mazoezi yake
"Mimi najitahidi sana kufanya mazoezi na kula vizuri huku nikiwa na ratiba maalumu ya kukutana na mpenzi wangu kimwili na sijawahi kutumia kilevi chochote kile " alisema Barnaba
Naye msanii wa filamu na bongofleva Shilole alisema anaonekana bado na mvuto kwa sababu ametenga masaa matatu ya kupumzika kila siku na hupendelea kula ugali samaki na mboga za majani
Alisema mbali na hilo pia anakuwa makini na chaguo la mafuta anayoyapaka ili aweze kuendelea kubaki na ngozi yake








