Muigizaji wa kike aliye juu katika filamu za Nollywood, Genevieve Nnaji alionyesha kupendeza na kuipendezesha sherehe ya kuzindua mfuko wa kusaidia yatima iliyoandaliwa na aliyekuwa Rais wa Nigeria, Chief Olosegun Obasanjo
Genevieve alikuwa kati ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo iliyofanyika jijini London, Ijumaa ya wiki iliyopita
Nyota huyo ambaye hakutarajiwa na wengi kuhudhuria hafla hiyo ghafla alionekana katika zulia jekundu maarufu kama red carpet akipigwa picha kabla ya kuingia ndani na kuungana na watu wengine waliohudhuria uzunduzi huo