Google PlusRSS FeedEmail

MSUVA KIPAJI KILICHOKUZWA THT




"MAZINGIRA yalinisababisha nipende kucheza muziki marafiki walionizunguka walinishawishi nijikite kwenye muziki, nje ya fani ya mpira ni mchezaji mzuri wa muziki hususani R&B" hayo ni maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na mcheza mpira wa timu ya Yanga Simon Msuva akielezea historia yake kabla ya kujiunga na mchezo huo ni kitu gani cha ziada alichokua anafanya

Alieleza  alianza kupenda kucheza muziki mwaka 2003 huku wakiwa wameunda kikundi chao hali iliyosababisha kupenda kufanya mazoezi na wachezaji wengine kutoka Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT), ingawa kwa kipindi hiko pia aliyumia muda wake wa kufanya mazoezi ya kucheza mpira kwani ilikuwa ni moja ya ndoto yake kuwa mwanasoka

Alisema alikuwa anapenda kucheza miondoko ya R&B kwa kipindi hicho ingawa kwa sasa anapenda kusikiliza na kupenda kucheza nyimbo tofauti zinazofanya vizuri katika tasnia hiyo ya muziki

Kutokana na hali ya kupenda kucheza muziki mchezaji huyo amejikuta kuwa na aina tofauti ya ushangiliaji pindi anapofunga goli, hali iliyopelekea mashabiki kujua staili yake ya ushangiliaji na kujisababishia kupata umaarufu zaidi katika mchezo wake

Kipindi chote alichokuwa akicheza dansi aliwahi kufanya shoo mbalimbali za kujificha na siyo zile katika majukwaa makubwa

Msuva aliweka wazi safari yake  mpira ambapo alianza safari hiyo mwaka 2004 katika shule za mpira mpaka mwaka 2010 alipojiunga na timu ya Taifa vijana wenye umri wa miaka 17 ambapo safari yake ya kwanza ilikuwa nchini Sudan

Kipaji chake kilianza kuonekana alipojiunga na timu ya Azam mwaka 2011 ambapo aliweza kukaa kwa kipindi cha miezi 6 na hatimaye kucheza mechi ya Uhai kapu ambapo aliibuka kuwa mfungaji bora

Alisema kuwa baada ya muda kidogo alipata 'shavu' lingine la kuchezea timu ya Moro United ambapo ni kama dirisha dogo kwake na ikampa nafasi ya kuzidi kuonekana ambapo timu ya Yanga ikamchukua hadi sasa anachezea Yanga

Siku za mapumziko anapenda kusikiliza muziki na kwenda (THT) kuangalia baadhi ya shoo na mazoezi yanayofanywa na madansa kwa ni moja ya vitu anavyovipenda

Pamoja na hayo aliweka mwanamke anayevutiwa naye kuwa ni mwanamke mwenye maumbile ya kike awe mweupe anayevutia kujiheshimu na kuthamini thamani ya mwanamke, hapendi mwanamke mwenye umbile kubwa yaani mnene

Aliongezea kuwa anapenda kuvaa rangi mbalimbali ingawa pinki, njano ni moja ya rangi anazozipenda, huku akivaa namba 7 ya raba aina ya Nike

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging