Google PlusRSS FeedEmail

MWANA FA AWA TISHIO


MSANII wa miondoko ya bongofleva Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' alionekana kuwa kivutio mbele ya mabinti katika uzinduzi wa video ya 'Me and U' ya msanii Ommy Dimpoz iliyofanyika
mwishoni mwa wiki Maisha club jijini Dar es Salaam

Mwana Fa alikonga nyoyo za mabinti baada ya kuimba nyimbo zilizoshika chati kwa miaka miwili iliyopita huku baadhi ya mashabiki kuonekana kuvutiwa na uimbaji wa msanii huyo pamoja na mashairi ya
nyimbo hizo Kibao ambacho kiliibua hisia kwa mashabiki na kumfanya aonekane bado kuwa kinara katika muziki wa bongo fleva

'Habari ndiyo hiyo' nyimbo aliyoshirikiana na AY baadhi ya mashabiki walionekana kuipenda shoo hiyo huku wakitamani muda uongezwe.

Akizungumza mmoja wa mashabiki hao Leyla Ally alisema kuwa nyimbo za zamani zinaradha nzuri ambazo kila mtu anatamani kusikiliza kwani zimejaa ubunifu wa hali ya juu

"Sisi tunataka nyimbo zinazoishi katika maisha yetu hebu angalia mistari ya nyimbo ya habari ndiyo hiyo imetoka muda mrefu kidogo lakini bado inafanya vizuri kila siku ," alisema Leyla

Aliongezea kuwa wasanii wanatakiwa kuwa wabunifu ili kazi wanazozitoa ziweze kufanya vizuri kwa kipindi chote hicho


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging