BAADA ya kupata ajali mbaya na kunusurika kufa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego afanya ibada ya kumshukuru mungu kwa kumuokoa katika janga hilo
Msanii huyo alipata ajali hiyo maeneo ya Mbuyuni jijini Dar es Salaam akiwa na gari yake aina ya Altezza yenye namba za usajili T762 CCQ alipogongwa na gari la aina ya Lori na baada ya hapo gari hilo kukimbia
Akizungumza na Maisha Ney alisema kuwa kutokana na ajali kuwa mbaya na ameona amenusurika kuumia na hata kupoteza maisha ameamua kumshukuru mungu kwa jambo hilo huku akisisitiza kila jambo linamipango yake
Alisema kuwa kitendo cha kutoka mzima kwenye ajali hiyo ni kitendo cha maajabu na kuona kuwa mungu anamakusudi yake na kuwataka watu wamuabudu na kumshukuru mungu kwa kila jambo
"Ajali ilikuwa mbaya na sasa tungekuwa tunazungumza mambo mengine kwani mzinga ulikuwa mkubwa tairi zote zilipasuka ni kitendo cha kumshukuru mungu nimetoka salamaa kwenye ajali hiyo zaidi ya kuteguka mguu lakini sasa niko salamaa" alisema Ney wa Mitego
Mbali na hayo alisema kuwa kutokana na bima yake kuwa ndogo na gharama za kutengeneza gari hilo kufikia milioni 6 anajikuta kusuasua kufanya marekebisho ya gari hilo mapema kwani garama ni kubwa
Msanii huyo alipata ajali hiyo katikati ya wiki iliyopita na gari lililomgonga lilikimbia na hata hivyo msanii huyo aliumia mguu ambapo sasa anaendelea vizuri huku mwenzake aliyekuwa naye pembeni aiumia na aliweza kulazwa hospitali lakini naye sasa anaendelea vizuri na teyari kasharuhusiwa